Azam TV yakanusha kuhusika na 'taarifa ya upotoshaji' kuhusu Ebola HD

21.05.2018
Kufuatia kipande cha video chenye kichwa cha habari kilichozua taharuki kuhusiana na taarifa za tahadhari ya Ebola mkoani Kigoma, Mkuu wa Kitengo cha Azam TV Online, Hassan Mhelela anatolea ufafanuzi nini hasa kilichotokea. TAARIFA Azam TV inautahadharisha umma kuhusu video yake iliyochapishwa na account moja kupitia YouTube kwa lengo la upotoshaji. Wakati video halisi ya Azam TV inataja hatua za tahadhari zinazochukuliwa na serikali mkoani Kigoma dhidi ya ugonjwa Ebola, wahusika wametumia video hiyo na kuandika kichwa cha habari tofauti kilicholenga kupotosha umma. Azam TV haihusiki na account hiyo ya YouTube na wala haina uhusiano wowote, haikutoa idhini kwa video yake kutumiwa na mtu au taasisi nyingine kupitia YouTube. Video yetu sahihi ni hii https://www.youtube.com/watch?v=KXVEGSKcIe4

Похожие видео