Jet Li's Fist Of Legend 1994: Jet Li vs Chin Siu Huo-Fight Scene
Ni Fight Scene kati ya Jet Li Vs Chin Siu Huo katika Movie ya Fist Of Legend: Baada ya Jet Li kurudi nyumbani (Jing Wu Temple) kutoka masomoni Japan-Kyoto University katika jiji la Kyoto, aliyeshika cheo cha Head Master katika Temple hiyo (Chin Siu Huo-Mtoto wa Master aliyekufa kwa njama ya kupewa sumu) pamoja na wazee wengine wa Temple wakakataa kumkaribisha pale Jet Li kwa sababu ya kuwa na mwanamke wa kijapani ambao ndiyo adui zao wakubwa kipindi hicho na kumtaka aidha amwache yule mwanamke (Mitsuko) au aachane na Jing Wu Temple akaishi na mwanamke wake kwingine. Lakini pia ujio mpya wa Jet Li ndani ya Temple ile kulifanya baadhi ya wanafunzi kujigawa, wengine kumsikiliza sana Jet Li na wengine kumsikiliza sana Head Master (Chin Siu Huo) kitu ambacho kilimuudhi Chin Huo. Ili kubaki na Head Master mmoja tu, Chin Huo akataka pambano kati yake na Jet Li na atakayeshinda ndiyo atakuwa Head Master mpya, na kama atashinda Jet Li atakuwa Head Master na yule mwanamke wa kijapan pia atabaki naye. Ingawa kabla ya pambano hilo Jet Li alishamwambia Chin Huo kuwa haitaji kuwa Head Master wa Temple, lakini Chin Huo hakukubali hoja hiyo na kumtaka lazima wapigane sababu wako wanafunzi ambao wameshaanza kumdharau. Jet Li akasema poa na pambano likapigwa kati ya Jet Li (Chen Zhen) na Head Master -Chin Siu Huo, hiyo historia fupi ya Fight Scene hii, enjoy-pata raha....!