UKWELI MTUPU Alikiba Afunguka Mazito Juu ya Mwanamke Aliyelala Nae HD
Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi1 Baada ya mitandao ya kijamii kulipuka vibaya kuhusu mrembo aliyepiga picha na staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ na wengi kudai kwamba wawili hao wana uhusiano, hatimaye msanii huyo ameibuka na kufafanua ukweli wa mambo. Picha ya Kiba na mrembo huyo waliyopigia hotelini, ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita hali iliyoleta sintofahamu huku kila mmoja akieleza kivyake. Kuna ambao walisema ndio mpenzi wake mpya, kuna wengine wakasema hafananii kuwa demu wake. “Hiki ndicho kifaa kipya bwana cha Kiba, si unaona alivyokikamatia…halafu hata mazingira yenyewe si unaona pale ni kitandani kabisa, huyu bwana ni mtu wake,” aliandika mdau mmoja katika mtandao wa Instagram. Wakati Global Tv online likiendelea kukusanya data za stori hiyo, lilikutana na chanzo kingine ambacho kilijiongeza zaidi kwa kutaka kuuaminisha umma kwamba picha hiyo ni ya kweli kwani mbali na hiyo iliyoonekana kama amepigia chumbani, kuna nyingine nyingi walizopiga pamoja. “Hii ishu nakwambia itakuwa na ukweli, japo Kiba si mtu wa kuanika sana mambo yake ya ndani lakini kwa hili kutakuwa na kitu maana mimi kuna picha nyingine ambazo naona Kiba amepiga na mrembo huyo,” kilifunguka chanzo hicho Global tv online lilifanikiwa kuzitia kibindoni picha zote za mrembo huyo akiwa katika mapozi tofauti na Kiba. Kuna ambazo walikuwa wamekaa, kuna nyingine walikuwa wamesimama huku mrembo huyo akiwa amemshika kiunoni Kiba. Grobal tv online lilimfikia rafiki mmoja wa Kiba ambaye alifunguka ukweli kuhusiana na picha hizo Kabla ya kuzungumza na Kiba. “Yule si mpenzi wake bwana. Ni dada yake na H Baba, ile picha walipiga Mwanza juzi walipokwenda katika Tamasha la Fiesta. Alifika pale kama shabiki wake, akaomba kupiga picha na Kiba, Kiba hakuwa na hiyana. “Tena zile picha zinazoonekana kama ni kitandani, wala si kitandani. Ni mapokezi ya hoteli ambayo walifikia wasanii wengi tu. “Na isitoshe ilikuwa rahisi sana kwa yule dada kukubaliwa kumfikia Kiba kwani ndiye anayeongoza kundi la WhatsApp la mashabiki wa Kiba Mwanza, kuna ile waliyosimama walipiga baada ya shoo,” alisema rafiki huyo wa Kiba. Global tv online lilimvutia waya Kiba ambapo alieleza kama ambavyo rafiki yake alifafanua kwa kirefu. Akaweka wazi kwamba yule ni shabiki wake mkubwa na kwamba alimuomba kupiga naye picha na hakuna kingine kilichoendelea. “Ni ujinga tu huo, hamna kitu chochote,” alisema Kiba. Alisema anashangaa kuona watu wanaihusisha picha hiyo na mazingira ya chumbani wakati inaonesha kabisa ni kochi la mapokezi ambapo mashabiki mbalimbali alipiga nao picha katika kochi hilo. Meneja wa msanii huyo, Aidan Seif alipozungumzia picha hizo alizidi kufafanua na kuwasihi Watanzania waache kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwachafua watu. “Ni ujinga tu huo watu wanafanya. Huyo dada ni dada yake H Baba na aliomba kupiga naye picha. Na si yeye tu, wengi walipiga naye picha lakini sijui nani ameanzisha hizo habari za kumchafua. Hamna chochote pale,” alis