"Mimi mtoto wa Ilala Kiingereza ni kukaza ulimi tu"-Kocha KILI STARS HD
Timu ya taifa ya Tanzania bara maarufu kama Kilimanjaro Stars iliyokuwa Kenya kwenye michuano ya Kombe la CECAFA Senior Challenge Cup leo imewasili Tanzania. Ni siku moja imepita toka icheze mchezo wake wa kukamilisha ratiba wa michuano hiyo dhidi ya timu ya taifa ya Kenya, Kilimanjaro Stars jana katika mchezo wake wa kukamilisha ratiba vs Kenya ilipoteza kwa goli 1-0 ikiwa ni mchezo wake wa tatu kupoteza wa hatua ya makundi katika michezo yake minne ikiwa imeambulia sare mchezo mmoja vs Libya na mitatu iliyosalia kupoteza.