Lipumba amlipua Mbunge wa CCM, "Alionekana ni Mbunge mzigo, hakutarajia kushinda kura za maoni 2020" HD

09.10.2018
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amemlipua mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Liwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Zuberi Kuchauka kwa kumtaja kuwa alikuwa ni mzigo ndani ya chama chao pia hakuwa na matarajio ya kushinda kura za maoni mwaka 2020. Kuchauka pia aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CUF kuanzia mwaka 2015 mpaka alipotangaza kuhamia CCM August mwaka huu.

Похожие видео