Wabunga wa Azimio wataka uteuzi wa Mithika Lintururi na Penina Malonza ukataliwe HD
Hatma ya watu walioteuliwa kujiunga na baraza la mawaziri itabainika wiki hii wakati kamati ya bunge kuhusu uteuzi itakapowasilisha ripoti mbele ya bunge itakayoelezea iwapo wanafaa kuhudumu kama mawaziri au la. Kamati hiyo inayoongozwa na spika wa bunge la taifa Moses Wetangula inaendelea kukamilisha ripoti hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa rasmi bungeni hapo kesho jumanne. Hata hivyo duru zinaarifu kuwa tofauti zimeibuka kati ya wanachama wa kamati hiyo kutoka mrengo wa Kenya Kwanza na ule wa Azimio kuwahusu baadhi ya walioteuliwa wakitilia shaka maadili yao. Kama anavyoarifu mwanahabari Geff Kirui upande wa upinzani unapendekeza uteuzi wa baadhi yao ukataliwe na bunge lakini wanachama kutoka mrengo wa Kenya Kwanza wakishinikiza uteuzi huo uidhinishwe. Join this channel to get access to perks: https://www.youtube.com/channel/UCKVsdeoHExltrWMuK0hOWmg/join Watch KTN Live https://www.standardmedia.co.ke/ktnnews/ Watch KTN News https://www.standardmedia.co.ke/ktnnews/ Follow us on http://www.twitter.com/ktnnews Like us on http://www.facebook.com/ktnnews