YANGA TV EPISODE 16: Kwani wao na sisi lini? Makambo na Tambwe wanamtaka yupi? HD
Kipindi cha Yanga TV Sehemu ya (Episode) 16, kilichoruka Ijumaa ya Septemba 28, 2018. Kuelekea mtanange wa wapinzani wa jadi, Simba SC vs Yanga SC (Mabingwa watetezi dhidi ya Mabingwa wa kihistoria) tunakuonyesha kile ambacho kikosi chetu kimekamilisha hadi sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania. Mabingwa wa kihistoria hadi sasa wana rekodi ya ushindi kwa 100/% kwenye Ligi Kuu; wamecheza mechi nne na wameshinda zote; kaumizwa Mtibwa Sugar, kalizwa Stand United, kagaragazwa Coastal Union kisha kabebeshwa maumivu Singida United; na hapa tulipofika tunauliza: “Kwani wao na sisi lini?” Tetesi kuhusu kadi za njano za kiungo Feisal Salum Abdallah limeelezwa humu. Unajua jirani zetu hawatukuti kwa idadi ya mashabiki? Acha kusema sema hovyo……kelele zote wanazopiga “hawatukaribii kwa idadi ya mashabiki” nah ii ni tafiti ya kisomi iliyothibitisha hilo. Tazama ujionee mwenyewe. Hii si Yanga ile iliyokuwa ikibezwa, hii imekuwa ni Yanga mpya, tena moto wa kuotea mbali. Tambwe ‘kazaliwa upya’, sasa waseme ‘Makambo na Tambwe wanamtaka yupiiiiiii? Tazama Yanga TV kwa taarifa za kina na uhakika kuhusu mabingwa wa kihistoria nchini. Yanga SC timu ya Wananchi. Yanga TV ni kila Ijumaa, saa 1:00 usiku Azam Sports 2