Sikiliza Mipasho ya Humphrey Polepole kwa Lowassa, Ataka Achukuliwe Hatua kwa Uchochezi HD
Polepole ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa kumekuwepo na upotoshwaji juu ya kauli ya Rais ya kutoruhusu watoto waliopata ujauzito shuleni kutorudi katika mfumo rasmi wa elimu. Polepole ameeleza kuwa wanaiunga kauli hiyo ya Rais Magufuli kutokana na tafiti mbalimbali ikiwemo tafiti ya mwaka 2006 ambayo inafafanua kuwa wanafunzi watakao pata ujauzito wakiwa shuleni hawatoweza kurudi katika mfumo rasmi wa elimu, hivyo wanahitaji kujiendeleza kielimu katika mfumo usiyo rasmi wa kielimu ikiwemo Mpango wa Elimu ya Msingi kwa waliyoikosa (MEMKWA), mfumo maalum unaotoa fursa ya kurudia mitihani kwa wanafunzi wa sekondari (QT) na vyuo mbalimbali vya ufundi nchini. Polepole amesema serikali haijaazimia kuwanyima elimu watoto wa kike kwani mifumo mingine isiyo rasmi ipo na wanaweza kuitumia, serikali inajitahidi katika suala la elimu ndiyo maana elimu ni bure kwa wanafunzi wa msingi na sekondari. Polepole ameongeza kuwa zaidi ya wanafunzi elfu 80 wapo nje ya mfumo wa elimu iliyo rasmi na wanaendelea na elimu zisizo rasmi za MEMKWA na QT, hivyo watanzania waelewe dhamira njema ya Rais. Katika hatua nyingine amelaani kitendo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa ambapo hakupenda kutaja jina lake na kueleza kuwa kauli aliyoitoa kwenye mualiko wa futari hivi karibuni inalenga kuchochea na kuwagawa watanzania kwa kuwagombanisha waislamu na serikali yao, hivyo kauli yake ipuuzwe kwani amewahi kutoa kauli ya ubaguzi wa kidini kipindi cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. Polepole pia amezungumzia suala la Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kutoa maoni yake ya kama katiba ingeruhusu kumuongezea muda wa utumishi Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi wake, Polepole amesema Rais Mwinyi ni mtanzania na anahaki ya kutoa maoni yake hivyo aachwe atoe maoni yake.