KAULI YA MWISHO YA DKT KALEMANI LEO KABLA YA KUTENGULIWA "AMSIFIA HAYATI MAGUFULI NA RAIS SAMIA" HD

13.09.2021
Leo September 12 majira ya saa nne usiku imetolewa taarifa ya mabadiriko ya baadhi ya Mawaziri ikiwemo taarifa ya aliyekuwa waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani kutenguliwa na nafasi yake kuchukuliwa na January Makamba Kabla ya taarifa hiyo kutolewa mapema leo Dkt Medard Kalemani alikuwa kwenye ziara akiwa mwenyeji wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati walipotembelea na kukagua mradi wa kufua umeme wa maji Rusumo uliopo Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera ambao utagharimu Dolla za Kimarekani Milioni 340 Na hii ni sehemu ya speech yake ya mwisho kabla ya kutenguliwa akiwa katika majukumu yake ya kiserikali

Похожие видео