Tenda Wema Nenda Zako HD
Akili ninywele na kila mtu ana zake! Ni msemo unaosimulia maisha ya mzee mmoja kutoka kijiji cha Keben kwenye Kaunti ya Kericho. Andrew Chirchir mwenye umri wa miaka 62 ameanzisha mradi wa kuhifadhi maji kwa wakaazi. Kinyume na matarajio ya wengi,kwa umri wake huo chirchir anaendelea kutumia ujuzi wa kitaalamu alio nao kuwapa huduma ya maji kwa wakazi bila malipo. Chirchir alishindwa kuendelea na masomo ya upili katika shule ya Londiani na kuamua kujiunga na chuo cha anuai cha Machakos….Kennedy Wandera na taarifa ya kina….