Tenda Wema, Nenda Zako HD
Ari, bidii na kutokuvunjika moyo...ndio maneno ambayo siku zote yamemwongoza maishani licha ya kuwa na mwanzo mbovu na mgumu....alifika darasa la nane tu lakini Daniel Musyoka sasa anajivunia shahada na stashada tano kutoka kwa mayatima...hata hivyo lengo lake ni kupata shahada 50 kutoka kwa watoto mayatima ambao amejitolea kuwasomesha. Pheona Kengah anateuelezea hadithi ya ujasiri na ndoto za musyoka ambaye amepata faraja kwa kuwatunza mayatima 186 huko kangudo ...