RUSSIA vs UKRAINE: UBALOZI WA UFARANSA, POLAND NA UMOJA WA ULAYA WATOA TAMKO RASMI.. HD

24.03.2022
RUSSIA vs UKRAINE: UBALOZI WA UFARANSA, POLAND NA UMOJA WA ULAYA WATOA TAMKO RASMI.. Kutokana na vita inayoendelea baina ya Ukraine na Urusi Ubalozi wa Ufaransa nchini pamoja na Umoja wa Ulaya (EU) umesema zinasimama na Ukraine katika kuhakikisha ya kwamba inamalizika kwa njia ya mazungumzo ili kuepuaka madhara zaidi yanayoweza kutokea. Taarifa iliyotolewa na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzaia Najil Hajloui pamoja na mabalozi wengine walioko nchini ambao nchi zao ziko kwenye Umoja wa Ulaya( EU.) inasema mnamo Machi 2,2022 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio ambalo linaitaka Urusi kusitisha mara moja matumizi ya nguvu dhidi ya Ukraine katika kura iliyoidhinishwa kwa wingi na nchi 141 ikiwa ni pamoja na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya huku nchi tano zikipinga na nchi 35 kuacha kupiga kura Kati ya wanachama 193 wa Jumuiya hiyo. Balozi huyo amesema Ufaransa na Umoja wa Ulaya zilijiunga karibu na Jumuiya zima ya Kimataifa katika kulaani vikali mashambulizi ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine anbapo ni shambulio kubwa zaidi juu ya Usalama wa Ulaya katika miongo kadhaa. Nikimnukuu katika taarifa yake balozi huyo amesema "Kukabiliwa na vita vilivyoanzishwa na Urusi bila uchokozi wowote ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za Kimataifa na ahadi zake zote,"amesema wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari akiwa na viongozi kadhaa wa Umoja wa Ulaya. Ameendelea kufafanua kuwa EU imeamua kuweka vikwazo vya moja kwa moja kwa watu wanaohusika na maamuzi yanayohusiana na vita lakini pia mfumo wa kiuchumi wa umma na wa kibinafsi wa Urusi ambao unaunga mkono juhudi hizo za vita na kwamba katika upande wa kifedha Urusi iko karibu kuondolewa kwenye masoko ya kifedha. ⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx ⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: https://www.youtube.com/playlist?list=PL22mc2rU91vDNQjLA5ikELAOcJp5XrakD ⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI? ⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982) ⚫️ Email: globaltvonlinenews@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: https://www.youtube.com/playlist?list=PL22mc2rU91vD-h-a328gR3qltQXYWVQiO ⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua ⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews ⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline

Похожие видео