Walichokisema UWT Kauli ya Rais Magufuli Kuhusu Wanafunzi Kupata Mimba HD
Baada ya Hivi karibuni Rais Magufuli Kutoa Tamko la Kuzuia Wanafunzi Wanaopata Mimba Kurudi Tena Shule Baada ya kujifungua, Umoja wa Wanawake Tanzania {UWT} Watoa Kauli ya Kumuunga Rais mkono Juu ya tamko Hilo. Tafiti Mbalimbali Zilizofanywa na Jumuiya na Taasisi za Hapa Nchini na Kimataifa Ikiwemo Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa {UNICEF}, Zinaonyesha Kuwa Mwanafunzi Mjamzito au Aliyejifungua ni Vigumu Kuendelea na Masomo Katika Mfumo wa Kawaida Ambao Umeandaliwa Kulingana na Saikolojia ya Mtoto Asiye na Jukumu la Malezi. Hivyo Kupendekezwa Mfumo Mbadala Kwa Wasichana Wajawazito Kuweza Kupata Elimu na Kujiendeleza Kupitia Mifumo ya MEMKWA, QT n.k, Ambayo Imewekwa Kitaaluma Ili Kumpa Fursa Msichana Kusoma Huku Akimhudumia Mtoto Wake. UWT Inatambua na Kuheshimu Mapendekezo ya Tafiti Hizo, Inawapongeza Wabunge Kwa Kupitisha Sheria Kali Kwa Wale Watakaowapa Wanafunzi Mimba, Kupinga Ndoa za Utotoni . Pia Inawashauri Wazazi , Walezi na Jamii Kwa Ujumla Kuwalinda Watoto wa Kike na Kutoa Elimu ya Kutosha kuhusu Masuala ya Jinsia , Athari za Mimba za Utotoni na Hatari ya Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa Ukiwemo UKIMWI. Mwisho UWT Inatoa Wito Kwa Wasichana Waliopo Mashuleni Kujidhatiti Kwenye Masomo na Kujiepusha na Vishawishi , Dira Yetu ni Kuwa na Taifa Lenye Uwiano na Fursa Sawa Baina ya Wanaume na Wanawake, Hivyo Wito Wetu ni Kuwataka Wasichana Wajitahidi Zaidi Ili Kufikia Lengo la Kuwa Washiriki Wakuu Katika Ujenzi wa Taifa.