Azam TV - Jinsi Rais Magufuli alivyowasilisha fomu kuhusu mali anazomiliki HD

28.12.2017
Rais Magufuli leo amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017

Похожие видео