HABARI AZAM TV 12/9/2018 HD

13.09.2018
Rais Magufuli aagiza malumbano baina ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Umma (DPP) yakomeshwe. Serikali Mkoani Mara imepokea hati kutoka kwa waliokuwa wakimiliki Hotel ya Musoma na Shamba la Mifugo zaidi ya 1300 la kiwanda cha Maziwa cha Utegi ikiwa ni agizo la Rais Dokta John Magufuli baada ya wamiliki hao kushindwa kuendeleza kwa muda mrefu. Wamiliki wa Mabasi Nchini TABOA wanatarajia kuanza kutumia tiketi za kielektroniki kuanzia juma lijalo huku kukiwa na mitizamo tofauti juu ya matumizi ya mfumo huu mpya unaotajwa utaondoa usumbufu wanaokumbana nao abiria kutoka kwa wapigadebe.

Похожие видео

Показать еще