Zitto apingana na Mnyika HD
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amepingana na wazo la John Mnyika, Mbunge wa Kibamba na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kuhusu kuwasilishwa kwa miswada mitatu inayohusu kulinda rasilimali za Taifa. Mnyika alilieleza Bunge kuwa si vyema kwa miswada hiyo nyeti kuwasilishwa na kujadiliwa kwa hati ya dharura na badala yake ni vyema wabunge wakapewa muda wa kuisoma kwa kina na kufanya tafiti, hata hivyo Zitto amesema Bunge halihitaji muda mrefu kuipitia miswada hiyo kwani mambo mengi yaliyomo yamekuwa yakisemwa tangu mwaka 2007.