IGP ataja magari yanayopaswa kupita barabara ya MWENDOKASI HD
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura ametoa ufafanuzi na kuyataja magari yanayopaswa kupita barabara ya magari yaendayo kasi maarufu kama Mwendokasi na kueleza sababu za kupita kwenye barabara hiyo. Wambura ameyasea hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Ijumaa Septemba 16, 2022 kwenye kikao cha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun kuhusu hali ya usalama nchini.