Wakazi wa Busia walalamikia msongamano wa matrela HD
Ukosefu wa sheria maalum za kuegesha magari umetajwa kama sababu kubwa ya msongamano wa matrela katika mji wa busia. baadhi ya wakazi wa busia wanalalamika kuwa kro hiyo inatatiza shughuli za uchukuzi na biashara baina ya mataifa ya afrika ya mashariki. wakazi hao wanaitaka serikali ya busia kushinikiza serikali ya kitaifa kupanua barabara hiyo na kuweka mahali maalum pa kuegesha matrela ili yaondoke kando ya barabara.wakazi hao wanalalamikia kuathirika kwa biashara mjini humo. kauli hizo zimetolewa wiki chache tu baada ya waziri wa uchukuzi james macharia kuzuru miji ya busia na malaba kutathmini hali.