ASKARI MPELELEZI ADAKWA KWA RUSHWA | Muungwana Tv HD

13.01.2020
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) mkoa wa Arusha imewafikisha mahakamani watuhumiwa 22 kwa tuhuma mbalimbali za vitendo vya rushwa katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2019. Mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha, Frida Wikesi akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu, Januari 13, 2020 amesema kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa hao kumetokana na ushirikiano mzuri wa raia wema ambao wapo tayari kutoa ushahidi mahakamani. Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao ni askari polisi, wafanyabiashara na watumishi wa umma na kwamba mashauri yao bado yanaendelea mahakamani katika hatua mbalimbali.

Похожие видео