Umaarufu wa kanisa la Roho Mafuta Pole kaunti ya Pokot magharibi HD

07.11.2020
Kanisa la Roho mafuta pole Afrika, lilipigwa marufuku na utawala wa mkoloni miaka ta hamsini. Kanisa hilo lililokuwa maarufu liliongozwa na Lucas Pkiech na lilihusika katika kuwapa waumini wa kiafrika imani ya kudhibiti mateso ya mbeberu. Miaka zaidi ya hamsini baadaye, Kanisa hilo sasa linaonekana kupata umaarufu katika kaunti ya pokot magharibi na mashariki ya Uganda, na kufanya viongozi wa kisiasa kuzuru dhehebu hilo kupata baraka. Collins Shitiabayi alizuru Kanisa hilo.

Похожие видео