Mafuta ya Mbegu za Mimea (Vegitable oils) na athari zake Unapozidisha HD

24.08.2017
Ni kweli mwili unahitaji mafuta ambayo hujulikana kama essential Oils, Omega 3 na Omega 6. Ingawaje ili uwe mwenye afya kiwango hiki kinatakiwa kiwe katika uwiano wa 1:1 au karibia na uwiano huo kumaanisha 1;4 au 1;3. Tafiti zinaonesha nyakati hizi sisi tunaosumbuka na maradhi yenye bila kuonekana kiwango cha Omega 3 na omega 6 kiko katika uwiano wa 1;16.7 kumaanisha kwamba tumekula kupindukia kiwango cha omega 6 kuliko omega 3. Kwa nini? Kwa sababu lishe yetu imesheheni kiwango kingi cha mafuta haya na kila vyakula tunavyo enda kununua vimepikiwa mafuta haya. Tizama maandazi keki,skonzi mojawapo wapo wa kiambata ni Vegitable oils,Alizeti,Pamba,Mahindi nk kila kona tunatumia kiwango kingi cha omega 6. Tumepiga teke vyakula vyenye kiwango kingi cha omega 3 ambavyo ni samaki,nyama,mayai,Flaxseed,almonds, na mafuta mengine mazuri kama Olive oil na Nazi ambavyo ni Ant inflammatory. Kwa ili kuzima moto unao endelea mwilini mwako Punguza mafuta ya Omega 6 na ongeza mafuta ya Omega 3. Tafiti zinasema kwamba ukiweza kupunguza hadi uwiano wa 1:4 unaweza kujikinga na magonjwa ya moyo kwa zaidi ya asilimia 50.

Похожие видео