TAARIFA ILIYOTUFIKI KUTOKA KWA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU BENJAMINI WILLIAM MKAPA
DODOMA: Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa ametoa rai kwa vyuo vya elimu ya juu hapa nchini kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika kufundisha na kufanya tafiti na bunifu mbalimbali ambazo zitakuwa msingi wa kuimarisha sekta ya elimu. Mkapa ametoa rai hiyo katika sherehe za kumsimika makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM, Prof. Faustine Karrani Bee aliyemteua mnamo tarehe 15 March mwaka huu.