Huyu Hapa KOCHA Mpya wa SIMBA SC Mrithi wa Mikoba ya SVEN, amewahi Kuifundisha AL AHLY ya Misri HD

09.01.2021
Mfaham kocha mpya wa SIMBA SC Mrithi wa mikoba ya SVEN #Sports AMEZALIWA Septemba 13,1973 ana umri wa miaka 47 ambapo nafasi aliyocheza mwenyewe zama za mpira alikuwa ni beki. Anaitwa Rene Weiler, raia wa Uswisi aliweka daluga kabatini 2001 alipokuwa anatumikia Klabu ya FC Winterthur. Anatajwa kuingia rada za Simba kuja kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye amebwaga manyanga ghafla. Sven aliamua kuacha kazi muda mfupi baada ya kupata ushindi mbele ya FC Platinum wa mabao 4-0 na kuipeleka timu hiyo hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Ameweka wazi kwamba sababu kubwa iliyomfanya asepe ndani ya kikosi hicho ni masuala ya familia. Mrithi wake ambaye anatajwa kwa sasa kuja Bongo alikuwa kocha ndani ya Klabu ya Al Ahly ya Misri ila kwa sasa yupo huru baada ya kufutwa kazi Oktoba mwaka jana.

Похожие видео

Показать еще